Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe (pichani) amezungumzia kukosekana kwa Katibu
Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa katika vikao vya chama hicho
vinavyoendelea jijini, akisema: “Nitazungumzia suala hilo muda muafaka ukifika.”
Mbowe alisema hayo jana katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach kilipokuwa kinafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema jana.
“Siwezi kusema zaidi ya hapo,”
alisema Mbowe alipoulizwa sababu za kutokuwapo Dk Slaa katika vikao
hivyo muhimu na kuongeza atatoa baadaye, mrejesho wa kikao hicho.
Kauli
hiyo ya Mbowe haikuondoa wingu zito lililotanda Chadema baada ya
kutoonekana hadharani kwa kiongozi huyo katika matukio manne muhimu ya
chama hicho kikuu cha upinzani, tangu waziri mkuu wa zamani, Edward
Lowassa ajiunge nacho.
Tofauti
na Dk Slaa, Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika alionekana jana kwa
mara ya kwanza katika kikao hicho na kufuta uvumi uliokuwa umesambaa
kuwa alikuwa na mpango wa kuachana na Chadema kama inavyodaiwa kwa Dk
Slaa.
Viongozi
hao walianza kutoonekana katika shughuli za chama tangu Lowassa
alipojiunga na Chadema Julai 28 na kukabidhiwa fomu ya kugombea urais
Julai 30 na juzi Agosti Mosi alipozirejesha.
Hata
hivyo, viongozi waandamizi wa Chadema wamesema suala la kutokuwapo kwa
Dk Slaa halipaswi kukuzwa kwa kuwa ‘anafanya kazi nyingine za chama.’
Alipoulizwa
jana, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema: “Suala la
kutokuwapo Dk Slaa ni kitu cha kawaida, anafanya kazi nyingine huko,
lakini pia kuna wasaidizi wake hapa ambao ni sisi manaibu. Mlikuwa
mnazungumzia Mnyika naye haonekani, si huyo. Hatuwezi kuendelea kujibu
‘rumors’ (uzushi) wa kwenye mitandao… nyie subirini si tupo mtaona kama
yupo au la.”
Mnyika atinga kikaoni
Jana, Mnyika alionekana katika viwanja vya hoteli hiyo lakini alikataa kuzungumzia kwa undani suala hizo.
“Siwezi kuzungumza chochote,” alisema Mnyika na hata alipoulizwa ni lini atawaeleza Watanzania juu ya kutoonekana kwake alisisitiza mara tatu kuwa “Siwezi kuzungumza chochote.”
Chama
hicho kinaendelea na mfululizo wa vikao vya vyombo vya juu ambapo leo
kinatarajia kutafanya kikao cha Baraza Kuu kabla ya Mkutano Mkuu kesho
kumpitisha mgombea wa urais kesho.
No comments:
Post a Comment