CHAMA cha
Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa kimetoa msaada wa vipaza sauti 18 (horn
speakers) kwa chama hicho jimbo la Iringa Mjini ikiwa ni sehemu ya
maandalizi ya kampeni za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25
mwaka huu.
Vipaza
sauti hivyo vilikabidhiwa jana kwa wajumbe wa halmashauri ya CCM ya
Manispaa ya Iringa waliokuwa na kikao maalumu cha maandalizi ya kampeni
za uchaguzi huo.
Akikabidhi
vifaa hivyo, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema
vimenunuliwa kwa Sh Milioni 36 zilizotolewa katika mfuko maalumu wa
kampeni za chama hicho mkoa wa Iringa.
Alisema
kwa kupitia msaada huo kila kata katika jimbo la Iringa Mjini itapata
kipaza sauti kimoja kitakachotumika kusaidia kampeni za madiwani, mbunge
na rais.
Mtenga
alisema CCM inaingia katika uchaguzi huo ikiwa na uhakika wa ushindi
mkubwa katika jimbo hilo ambalo kwa miaka mitano iliyopita lilikuwa
likiongozwa na Mchungaji Peter Msigwa aliyechaguliwa kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Pamoja
na matumaini hayo makubwa, Mtenga aliwataka viongozi na wanachama wa
chama hicho kufanya kazi ya kisiasa ili lengo hilo litimie.
“Jimbo
la Iringa Mjini linawapiga kura zaidi ya 100,000; pamoja na kuwa na
mikakati inayotuhakikishia ushindi hatutakiwa kulala, tunatakiwa kuwajua
wapiga kura waliko, tuwafuate na tuwaeleze kwanini Mchungaji Msigwa
hastahili kurudi tena bungeni,” alisema.
Naye
Katibu wa CCM Jimbo la Iringa Mjini, Elisha Mwampashi amesema baada ya
mchakato wa kura za maoni kumalizika na uteuzi wa wagombea kufanywa,
wapo baadhi ya wana CCM ambao kwa matendo yao wanaonekana kuwa na
mipango ya kukisaliti chama hicho.
“Wapo,
wengine walikuwa wagombea wa nafasi mbalimbali na wengine ni viongozi na
wanachama amabo hatupo nao kikamilifu wakati tukielekea katika uchaguzi
mkuu” alisema.
Mwampashi
alisema CCM haitakiwa kuwavumilia wanachama wa aina hiyo na akawaomba
wajumbe wa halmashauri hiyo kutoa taarifa za wanachama wasaliti ili
waweze kushughulikiwa.
Akishukuru
kwa msaada huo, Mwenyekiti wa CCM Manispaa ya Iringa, Abeid Kiponza
alisema; “vinatakiwa kutumika kwa kazi iliyokusudiwa, na kazi hiyo si
nyingine zaidi ya kukiletea ushindi Chama cha Mapinduzi.”
Wakati
huo huo, Kiponza amewataka wagombea udiwani, ubunge na viongozi wa ngazi
mbalimbali wa chama hicho kuvaa sare za chama hicho katika kipindi
chote cha kampeni.
“Sitaki
mavazi yenu ya disco, na mgombea au kiongozi anayeogopa kuvaa sare za
chama, akae nyumbani kwake,” alisema katika kikao hicho ambacho pia
waliokuwa wagombea udiwani na kuuanguka katika mchakato wa kura za maoni
walitangaza kuvunja makundi.


No comments:
Post a Comment