Msajili
wa Bodi ya Wahandisi nchini Tanzania (ERB) Muhandisi Steven Mlope
akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea
mafanikio ya Bodi hiyo katika kipindi cha miaka 10 hasa ukuzaji wa sekta
ya ajira nchini Tanzania.
Bodi
ya Usajili wa Wahandisi nchini Tanzania (ERD) imefanikiwa kutengeneza
ajira 1600 kwa Watanzania kufuatia usajili wa makampuni 160 ya ushauri
wa kihandisi yaliyoanzishwa nchini kote nchini katika kipindi cha miaka
10 kuanzia mwaka 2005 hadi 2015.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuelezea mafanikio ya
Bodi hiyo kwa kipindi cha miaka 10 Msajili wa Wahandisi nchini Tanzania
(ERB) Muhandisi Steven Mlope amesema kuwa kwa kusajili makampuni 160
katika kipindi cha miaka 10 pia wamefanikiwa kusajili wahandisi wapatao
8496 ambao kwa ujumla wao wametengeneza ajira kwa Watanzania 256,480.
Amesema
katika kipindi cha miaka 10 Bodi hiyo imefanikiwa kuongeza kwa kiasi
kikubwa idadi ya wahandisi waliosajiliwa kutoka 6868 waliokuwepo nchini
Tanzania hadi 15,364 mwaka 2015.
Aidha
Muhandisi Mlope amesema kuwa Fani ya Uhandisi nchini Imeendelea kukukua
kutokana na uwepo wa wahandisi wa Majengo,wahandisi wa mazingira,
Mifumo ya kompyuta na wahandisi wa mazingira wanaofanya kazi zao kwa
kushirikiana.
Aidha,
amesema kuwa Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa kuzingatia sheria ya
Bunge namba 15 ya mwaka 1997 iliyofanyiwa marekebisho, na sheria No.24
ya mwaka 2007 imepewa majukumu ya kuratibu na kusimamia mienendo na
shughuli za Kihandisi zinazofanywa na wahandisi pamoja na makampuni ya
ushauri wa kihandisi nchini.
Ameongeza
kuwa kwa mujibu Sheria ni kosa kwa mtu binafsi,kikundi cha watu
binafsi, kikundi cha watu au kampuni yoyote kutoka ndani na nje ya nchi
kufanya shughuli za kihandisi bila kusajiliwa au kuwa na wahandisi
wasiosajiliwa.
Ameeleza
kuwa katika kipindi cha mwaka 2005 hadi 2015 Bodi hiyo ilitoa onyo na
adhabu mbalimbali ikiwemo kufuta usajili wa wahandisi 330 waliokiuka
Sheria ya Bodi ya Usajili wa wahandisi.
Kwa
upande wa shughuli za kihandisi katika ngazi ya wilaya kote nchini
Muhandisi Mlope amesema kuwa kufikia mwaka 2015 hali imeendelea
kuimarika licha ya kuwepo kwa changamoto ndogondogo.
Muhandisi
Mlope amebainisha kuwa Bodi inaendelea kuratibu mpango wa Mafunzo
(SEAP) wenye lengo la kuwajengea uwezo wahandisi wanaohitimu masomo
katika vyuo mbalimbali ili waweze kukidhi viwango kuwawezesha vya
kuwawezesha kusajiliwa na Bodi hiyo.
“Mpango
huu wa mafunzo unaofadhiriwa na Serikali kwa lengo la kuwajengea uzoefu
wahitimu, kuwawezesha kuajiliwa na kupata uzoefu mapema umekuwa na
manufaa makubwa kwa nchi yetu”
Ametoa
wito kwa wenye viwanda na makampuni kuwapokea na kuwaajili wahandisi
waliosajiliwa na wale waliokula kiapo ili kazi wanazozifanya ziweze
kukidhi viwango vilivyowekwa.
Pia
amesema kuwa Bodi hiyo inaendelea kuwaendeleza wahandisi wataalaam
waliopo nchini kwa kuandaa mihadhara na kozi fupifupi ambazo huendeshwa
na vyuo vinavyotoa mafunzo ya kozi hiyo huku wao kama bodi wakitoa
ithibati na kuandaa makongamano ya wahandisi kila mwaka.
Amefafanua
kuwa Septemba 3 mwaka huu Wahandisi watakuwa na Kongamano kubwa la
mwaka litakalowakutanisha wahandisi wote nchini ili kuweza kukidhi
matarajio ya Wananchi kufuatia wengi wao kuongeza uelewa juu ya matumizi
ya wahandisi.
“Mwamko
sasa umeongezeka kutokana na Serikali kuendelea kuweka mkazo katika
masomo ya Sayansi na ujenzi wa maabara ili kuzalisha wataalam wa kutosha
wenye viwango” Amesema.
Kuhusu
maslahi ya wahandisi nchini amesema kuwa wao kama Bodi wanaishukuru
Serikali kwa kuendelea kuboreshaji maslahi yao na kusisitiza kuwa jambo
hilo linaendana na mabadiliko ya uchumi yaliyopo ili kuwawezesha
wataalam hao kufanya kazi zao kwa ufanisi na kuheshimiwa na jamii
wanayoitumikia.
No comments:
Post a Comment