Abiria
wakishuka toka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania
(ATCL) katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni
SHIRIKA
la ndege la taifa (ATCL) limerejesha safari zake kuelekea mkoani Mwanza
ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua huduma kwa wateja wake
hapa nchini.
Safari ya
kwanza ya shirika hilo kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa
juma lilopita kwa kukutumia ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari
hizo kusimama tangu mwezi Agosti mwaka mwaka jana.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja
wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily
Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari hizo umezingatia mahitaji
ya wateja wa shirika hilo.
“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha majiji haya mawili. Kwa kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini tukafanya kila jitihada kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini Mwanza,’’

alibainisha Fungamtama huku akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.
Alisema
ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya
ndege yanayofanya safari zake kuelekea mkoani humo, shirika hilo
limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba na kutoa huduma
zake kwa gharama nafuu.
Akizungumzia
na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja
wa ndege wa Mwanza mmoja wa abiria waliosafiri na ndege hiyo Bw. Bakari
Hamidu mbali na kushukuru kurejeshwa kwa huduma hiyo pia alionyesha
kuridhishwa kwake na ubora wa huduma unaotolewa na wahudumu wa shirika
hilo.
“Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ alisema Bw. Hamidu.
“Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ alisema Bw. Hamidu.
Pamoja na
kurejesha safari hizo za mkoani Mwanza, shirika hilo pia kwa sasa
linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya
Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100.
“Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam’’ aliongeza Fungamtama.

No comments:
Post a Comment