Mkazi wa Cibitoke akikimbia ghasia zilyozuka wakati wa operesheni ya polisi ya tarehe 1 Julai.
Na RFI
Shirika
la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International
limesema maafisa wa usalama nchini Burundi wamekuwa wakitumia vyuma na
tindikali dhidi ya wafuasi wa upinzani.
Amnesty
inasema ushahidi umeonesha kuwa polisi na maafisa wa ujasusi wamekuwa
wakitumia mbinu hizo kuwalazimisha wafuasi wa upinzani kukiri taarifa
wanazozitaka.
Polisi pia wameshtumiwa kuwapiga wafuasi hayo na nyaya za umeme na kuwalazimisha kuinamisha vichwa vyao ndnai ya maji chafu.
Mwanamume mmoja amesema alifungiwa dumu la mchanga katika sehemu zake za siri kwa nusu saa hadi akazirai.
Hata
hivyo mauaji yamekithiri nchini Burundi hasa katika mji mkuu wa
Bujumbura, ambapo watu wanauawa kila kukicha. hali hii imepelekea raia
kuanza kukimbilia katika nchi jirani, husuan nchini Rwanda.
Je kuna raia wa Rwanda ambao hukamatwa Burundi?
Hivi
karibuni serikali ya Rwanda imewaonya viongozi wa Burundi na kuwataka
kuwaachilia huru raia wake wanaokamatwa na kupelekwa sehemu
isiojulikana. Mashahidi wanasema kuna raia wa Rwanda ambao hivi karibuni
walitereshwa ndani ya basi ziliyokua zikitokea Rwanda zikielekea
Bujumbura. Mashahidi wengine wamebaini kwamba kuna vizuizi ambavyo
vimewekwa katika eneo la Bugarama, mkoani Muramvya, ambapo kila gari ya
uchukuzi inapofika sehemu hiyo abiria wote hullazimishwa kushuka na
kuonyesha kadi zao za uraia, huku wakifanyiwa msako. Inaarifiwa kuwa
vizuizi hivyo hulindwa na askari polisi na vijana ambao wanasadikiwa
kuwa ni kutoka chama tawala cha CNDD-FDD, Imbonerakure.
Viongozi
wa Burundi hawajaeleza lolote kuhusu onyo hilo kutoka Rwanda. hali ya
wasi wasi imeendelea kutanda katika maeneo mbalimbali nchini Burundi.
Hayo
yakijiri, idadi ndogo ya wapiga kura wamejitokeza Jumatatu wiki hii
kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa, nchini Burundi.
Uchaguzi
huu unakuja siku chache tu baada ya rais Piere Nkurunziza kuapishwa
baada ya kushinda uchaguzi weenye utata uliokosolewa kimataifa.
No comments:
Post a Comment