Maofisa wa polisi wakiwa eneo la tukio lilipotokea shambulio lililoua watu 14 usiku wa kuamkia leo.
Takribani watu 14 wameuawa, 11 wakijeruhiwa baada ya Al-Shabaab
kushambulia kijiji cha Soko Mbuzi kilichopo jirani na Mji wa Mandera
nchini Kenya usiku wa kuamkia leo. Mamlaka husika huko Mandera
yathibitisha.Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa shambulio lilitokea saa 7 usiku wa kuamkia leo wakati wakazi wa Kijiji cha Soko Mbuzi wakiwa wamelala.
Shambulio hilo limeelezwa kuwalenga wafanyakazi wa machimboni ambao wengi wao siyo wenyeji.
Taswira kutoka Kijiji cha Soko Mbuzi lilipotokea shambulio.
Wananchi wakiwa eneo hilo la tukio.





No comments:
Post a Comment