WATU zaidi ya 10 wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Maendeleo na
Demokrasia (CHADEMA) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejeruhiwa katika
mapigano, yaliyosababishwa na mabishano ya kisiasa wakati wakinywa
pombe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana mjini hapa, tukio hilo lilitokea
katika kijiji cha Kegonga tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara.
Imeelezwa kuwa miongoni mwa majeruhi ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Magamaga, Mohere Nyamhanga ( Chadema).
Kwa mujibu wa mtoa taarifa, ugomvi wa mapanga ulizuka baada ya
mabishano ya kisiasa kuibuka wakati watu hao walipokuwa wakijipatia
vinywaji katika grosari ya Mwalimu Mwita Mohere.
Imeelezwa kuwa baadhi ya majeruhi wamelazwa katika vituo vya afya vya Mriba na Masanga.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii huku akiwa na jeraha la
mgongoni, la kupigwa na kitu kizito, Mwenyekiti wa Kitongoji cha
Magamaga kupitia Chadema, Mohere Nyamhanga alisema wakati wakijipatia
kinywaji kulizuka mabishano ya kisiasa yaliyoibua hisia kali.
Alisema alipojaribu kuzuia mtafaruku, alipigwa jiwe mgongoni na
kuumia. Mwenyekiti huyo wa Kitongoji aliwataja wafuasi wa Chadema
waliojeruhiwa kuwa ni pamoja na yeye mwenyewe, Nyangi Chacha na Magasi
Mwita.
Kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi alitaja walioumia kwa kukatwa
mapanga kuwa ni pamoja na Marwa Mohere, Nyamaretio Mwita na Pius
Nyarengwa.
Baadhi yao watu hao wamelazwa wakiwa na majeraha makubwa katika vituo vya afya vya Mriba na Masanga.
Baadhi yao watu hao wamelazwa wakiwa na majeraha makubwa katika vituo vya afya vya Mriba na Masanga.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya, Lazaro Mambosasa alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuwaasa wanasiasa kuwa waangalifu na
kuvumiliana.
“Jeshi letu linawaomba viongozi wa vyama vya siasa kutoa elimu kwa
wafuasi wao kuendesha siasa kwa amani na bila kuingiliana na vyama
vingine”, alisema Kamanda Mambosasa.
No comments:
Post a Comment