Mwanasheria
Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata
wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na
chama hicho.
Lissu
ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa
CHADEMA ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio
wa Lowassa ndani ya CHADEMA.
Akizungumza jana na waandishi wa habari Lissu alisema,
“Kama
wapo watakao jiondoa CHADEMA, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi
ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze. Mfumo
tawala unabomoka vipande vipande. Unapobomoka, dalili zake ni watu ambao
wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”
“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.
"Tunamkaribisha
kwetu siyo kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu
tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia
Mawawi, Nigeria na Kenya”
Akizungumza kuhusu CHADEMA kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu alisema;
“…hatukuwa
na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa
Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe
aliwajibika.”
“Alijiuzulu
Uwaziri Mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya
mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais
“tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje? Hilo ni vumbi,
litakapotulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka,
tutajenga nchini. Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,”
No comments:
Post a Comment