THEA AFURAHIA MAISHA NJE YA NDOA - LEKULE

Breaking

13 Jul 2015

THEA AFURAHIA MAISHA NJE YA NDOA

Kutoka moyoni! Staa wa sinema za Kibongo, Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka kuwa anafurahia maisha anayoishi bila ndoa kwani anafanya mambo kwa uhuru na hana msongo tofauti alivyokuwa akiishi kwenye ndoa na aliyekuwa mumewe, Michael Sangu ‘Mike’.

Thea ambaye kwa sasa anapatikana kwenye Kundi la Sanaa la Kaone, alisema hakuna kinachomuumiza kuishi bila mume kwani ni mtu ambaye wamekutana ukubwani hivyo kuachana ni jambo la kawaida.
“Nafurahia sana maisha bila ndoa, sina stress (mawazo) kama zamani, nafanya mambo yangu kwa uhuru mkubwa na simuwazii mtu kabisa tofauti na kwenye ndoa, mara sijui umuwazie mtu mzima mwenzako, mara sijui vile, acha nitafune maisha,” alisema Thea.

No comments: