The Rock ameweka wazi sababu za yeye kuacha mchezo wa mieleka… - LEKULE

Breaking

1 Jul 2015

The Rock ameweka wazi sababu za yeye kuacha mchezo wa mieleka…

Dwayne  Johnson maarufu kama The Rock ni mwigizaji, movie producer na mchezaji mieleka kutoka Marekani aliejitengenezea jina kubwa kwenye mieleka na kufanya apate shavu kubwa kwenye movie za action HollywoodMarekani.
The Rock alichukuwa time na kufanya interview na gazeti la Marekani Esquire na kuongelea mambo mengi ikiwemo sababu zilizomfanya aingie kwenye tasnia ya uwigizaji pamoja na mafanikio yake binafsi. The Rock alikuwa na haya ya kusema:
Dwayne Johnson kwenye movie ya The Expendables 3 ambayo ndani Bruce Wills ameonekana pia.
Kuhama kwenye mieleka kwenda kwenye uwigizaji:“Baada ya kufanikiwa kwenye mieleka, nilihamasika kujabiru uwigizaji wa movie za action, na nimefika hapa nilipo kwa kutumia nidhamu niliojinfunza kwenye mieleka, kujenga ukaribu na watu kwenye industry, na kujiunga na madarasa ya kuigiza”.
Dwayne Johnson kwenye movie nyingine kali ya G.I. JOE Retaliation.
Kama anapendelea uwigizaji zaidi kuliko mieleka:Mieleka ni mpenzi wangu wa kwanza, lakini kwenye uwigizaji kuna upendo tofauti ambao unaniruhusu mimi kugusa watu kupitia sanaa nyingine na pia kutengeneza hela ndefu zaidi, movie zinanifundisha mambo mengi sana ambayo nisingeweza kuyajua mwanzoni”.
Hapa ni kwenye movie aliyoigiza mwaka huu SAN ANDREAS, movie iliofanya vizuri Marekani.
Kama alichukuliwa serious alivyoanza kuigiza: “Haikuwa rahisi hapo mwanzoni, kama Anorld Schwarzenegger niliambiwa nina mwili mkubwa kuwa mwigizaji wa movie za action na nilinyimwa nafasi nyingi lakini sikukata tamaa, na leo niko hapa kwa sababu sikuchoka”.

No comments: