KAMPUNI
ya Jambo Concepts (T) Ltd, inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa
Spoti na Jarida la Jambo Brand, limempoteza mfanyakazi wake mwingine wa
idara ya masoko, Kinai Mtinda (pichani), baada ya kufariki dunia saa 7
usiku wa kuamukia leo katika Hospitali ya Sinza Palestina jijini Dar es
Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Msiba na
mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa kaka yake Mbezi Beach na
taratibu zingine kuhusiana na msiba huo zitatolewa baadae.
Marehemu Kinai ameacha watoto wawili.
Kifo cha
Mtinda kinakuja ikiwa ni siku chache tangu afariki dunia Meneja Mkuu wa
Kampuni hiyo, Ramadhani Kibanike mwishoni mwa mwezi uliopita. Bwana
alitoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe Amina



No comments:
Post a Comment