Shilole na Nuh Mziwanda Wapigana Chini..........Mziwanda Amwita Shilole ASHA NGEDERE - LEKULE

Breaking

19 Jul 2015

Shilole na Nuh Mziwanda Wapigana Chini..........Mziwanda Amwita Shilole ASHA NGEDERE


Ile couple ya wasanii wa kibongo wasioishiwa skendo, Shilole na Nuh Mziwanda imeubuka upya kwa staili ya kipekee.

Tumezoea kusikia Shilole kamnasa makofi Mziwanda, mara kampiga chupa na mengine mengi ya aina hiyo.

Awamu hii wamekuja na mpya ya kuchambana live mitandaoni. Nuh kafananishwa na ganda la ndizi huku Shilole akifananishwa na Asha Ngedele......

Aliyelianzisha Varangati hili ni Shilole, ambaye ameandika ujumbe huu instagram.

"Mwanaume hata umfanyie nini haridhik lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakin mh! Nimejitahid nimehangaika'ila sasa kama gari limewaka'aka babu weeee kanikuta na maisha yangu wacha niendelee na maisha yangu'Mimi na yeye baaaaaaasi #GaNdALaNdiZi .™@shilolekiuno"

Nuhu nae akaona isiwe tabu akamwaga ugali, na kachumbari

"Mwanaume wa kweli ukaa kimya'sibishani na upumbavu'mwanamke asieridhika na kujua kua kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa'na kuvumilia mambo yote alionifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu'familia na'wasanii wenzangu na wadau'anaanza kunitukana mitandaoni for whaaaat!!! Mxeeeeew'mimi bado kijana na nna time ya kupata maisha yangu na mtu atakae thamini moyo wangu 'nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari 'mimi nacheka tu #AsHaNgeDerE. ™@mziwandanation"


No comments: