Rais Wa FC Barcelona Atoa Kali Ya Mwaka - LEKULE

Breaking

8 Jul 2015

Rais Wa FC Barcelona Atoa Kali Ya Mwaka

Raisi wa klabu ya Barcelona Josep Bartomeu ameonyesha dhamira ya “Sizitaki Mbichi Hizi” baada ya kuuthibitishia umma walikua hawana mpango wa kumsajili kiungo kutoka nchini Ufaransa pamoja na klabu bingwa nchini Italia, Juventus, Paul Pogba.
Bartomeu, amesema ilikua ni kama bahati mbaya kwao kujikuta katika wimbi la kutaka kumsajili kiungo huyo katika kipindi hiki, lakini kulikua hakuna mipango yoyote kwao kumpa kipaumbele mchezaji huyo.
Amesema licha ya vyombo vya habari kuripoti kwa kiwango kikubwa kuhusu mikakati ya usajili waliokua wamejiwekea kwa Pogba, kulikua hakuna msukumu miongoni mwa viongozi klabuni hapo ambao ungesaidia usajili wa kiungo huyo.
Hata hivyo kauli ya kiongozi huyo wa ngazi ya juu huko Camp Nou, imepokelewa na wadau wa soka duniani kote kama hadithi ya Sungura iliyokua imenakshiwa na sentensi ya “Sizitaki Mbichi Hizi” kutokana na hamu kubwa iliyokuwepo ya kuona Pogba anaitumikia Barcelona msimu ujao.
FC Barcelona walishindwa kuendelea kufanya mazungumzo na viongozi wa Juventus juma lililopita, baada ya kushindwa katika suala la ada ya usajili ambapo viongozi wa The Bianconeri walihitaji zaidi ya pound million 50 lakini Barca hawakuonyesha kuwa tayari kutoa kiasi hicho cha pesa.

Klabu za Real Madrid, Chelsea pamoja na Manchester City zinaendelea kutajwa na vyombo vya habari katika harakati za kumuwani Pobga ambaye ada yake ya usajili unakadiriwa kufika kiasi cha paund million 70.

No comments: