Dar es Salaam.
Sasa ni wazi; mmoja kati ya Dk John Magufuli, Dk Asha Rose Migiro au Balozi Amina Salum Ali atapeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu ujao baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kukamilisha kazi yao ya kupiga kura usiku mwingi wa kumkia leo.

Licha ya mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya
Kikwete kutangaza kuwa matokeo ya kura hizo yatatangazwa leo saa 4:00
asubuhi kuna kila dalili kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk Magufuli ndiye
atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Lakini ushindi wa Dk Magufuli unakabiliwa kikwazo kikubwa kutoka kwa makada hao wawili wanawake na wanadiplomasia.
Watatu
hao walifanikiwa kuingia hatua hiyo ya mwisho ya kupigiwa kura na
mkutano mkuu baada ya kuwabwaga makada wengine wawili, Bernard Membe,
ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa kutokana na Waziri Mkuu wa zamani,
Edward Lowassa kuenguliwa na Kamati Kuu juzi, na January Makamba katika
kura zilizopigwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu.
Awali
kabla ya kupigiwa kura na Mkutano Mkuu jana, Kikwete aliwataka wajumbe
kumuunga mkono mgombea atakayepitishwa kupeperusha bendera ya chama
hicho na kuachana na makundi.
“Wagombea wapo watatu na
wote wana sifa za kuwa Rais. Halmashauri Kuu imewapitisha kwa
kujiridhisha na tabia na mienendo yao na atakayepitishwa ataiongoza nchi
yetu vizuri. Anatakiwa apatikane Rais zaidi yangu ili tusonge mbele.
Tunataka rais atakayefanya mambo zaidi yangu,” alisema JK.
“Tumevuka
hatua ya makundi na sasa tunatafuta mgombea wa chama na si mgombea wa
kundi au mgombea binafsi. Wagombea urais waliojitokeza walikuwa 38 na
makundi lazima yalikuwa mengi. Tukipata mgombea mmoja makundi yanatakiwa
kuyeyuka.”
Hisia za wajumbe kwa Dk Magufuli
zilionekana wazi wakati makada hao walipopewa dakika 15 za kujieleza
mbele ya Mkutano Mkuu, huku mwenyekiti akiweka sharti la kuzuia
kushangilia hata kama wakiguswa. Lakini sharti hilo lilionekana
kuwasumbua wajumbe hao na mara kwa mara wakajikuta wakilipuka na
kushangilia.
John Pombe Magufuli
Akijinadi
kwenye mkutano huo, Dk Magufuli, ambaye alizungumza kwa dakika tisa
kuanzia saa 5:55 hadi saa 6:04 usiku, aliwashukuru wajumbe wa mkutano
huo, wakiwamo wageni waalikwa na muda huo wajumbe wakaanza kumshangilia.
“Naombeni
kura kwa sababu ninaamini kuwa nitafanya kazi na nyinyi na mtanituma na
nitakuwa mwakilishi wenu na nitailinda CCM katika kushinda kikamilifu
na kushika dola ili kuiongoza nchi hii. Nitadumisha Muungano wetu,”
alisema Magufuli.
“CCM imenilea na ninawaahidi wajumbe
sitawaangusha. Nimefanya kazi na Rais Kikwete na nadhani sikukuangusha.
Umenituma katika kipindi chote cha miaka 10 na nilidhani leo utataka
nielezee barabara ulizonituma wewe.”
Magufuli alisema
anatamani kueleza jinsi alivyojenga madaraja, barabara, lakini hawezi
kwa kuwa mkutano huo ni wa kuomba kura na akafafanua kuwa kazi ya
uongozi ni ya kupokezana vijiti.
“Viongozi waliopita
wamefanya kazi nzuri na mimi nafarijika kuona nimejifunza vya kutosha
katika kipindi hicho na sitawaangusha na nina uhakika hapa
ninapozungumza wapinzani huko walipo wapo matumbo joto maana maendeleo
hayana chama ila lazima yaletwe na chama kinachojua kujisimamia,”
alisema.
Magufuli aliwageukia viongozi wakuu wa CCM
waliokuwa wamekaa meza kuu na kuwaomba kura sambamba na wajumbe wengine
wa mkutano huo, baada ya hapo aliwapa mikono viongozi hao na kuimba
kidogo kupitia kipaza sauti.
Amina Salum Ali
Balozi Amina, ambaye alizungumza kwa dakika 11 kuanziaa saa 5:35 mpaka saa 5:46 usiku, alieleza uzoefu wake wa miaka 38 ya utumishi ndani ya CCM na miaka 42 ya utendaji serikalini.
Alisema amelelewa na viongozi wakuu wa chama hicho akiwamo Rais Kikwete na kufafanua kuwa hana kundi ndani ya CCM hivyo atawaunganisha na kuwa kitu kimoja.
“Naomba mnichague ili tutoke Dodoma tukiwa na ushindi. Taifa letu lipo katika uchumi wa kati na tunatakiwa kwenda katika uchumi wa juu hivyo ni lazima tuendeleze mazuri yaliyofikiwa na Serikali ya Awamu ya Nne,” alisema.
Kuhusu Muungano alisema ataudumisha kwa kila hali na kusisitiza kuwa Muungano hauwezi kudumishwa kama chama hakitakuwa na viongozi imara.
Kilipofika kipindi cha maswali, hakuna mjumbe hata mmoja wa mkutano huo aliyejitokeza kumuuliza swali kama ilivyokuwa kwa wagombea wote watatu ambao hawakuulizwa maswali.
Asha-Rose Migiro
Dk Migiro, ambaye kipaumbele chake ni kukuza uchumi utakaowafikia Watanzania wengi, alizungumza kuanzia kwa dakika tano tu kuanzia saa 5:48 mpaka saa 5.53 usiku.
Alisema kwa kutumia uzoefu wake wa uongozi na elimu atadumisha na kusimamia Muungano na mchakato wa kupata Katiba Mpya na kwamba ataongoza nchi kwa kufuata ilani ya CCM.
“Nipeni ridhaa yenu ili niweze kuipeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu huu. Nipeni kura usiku huu ili niweze kusonga mbele,” alisema Migiro.
Membe amfuata Lowassa
Awali jana usiku, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC) ilipitisha majina matatu ya makada wanaowania urais kwa tiketi ya chama hicho, ikiwa imeandika historia mpya kwa kupitisha kwa mara ya kwanza wanawake wawili, huku kigogo mwingine, Bernard Membe akitemwa.
Dk John Magufuli, Dk Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali ndio waliopita kwenye mchujo huo wa Halmashauri Kuu na majina yao kupelekwa kwenye Mkutano Mkuu ambao ulianza saa 3 usiku.
Kada mwingine aliyekuwa amepita kwenye tano bora juzi, January Makamba, hakufurukuta mbele ya Halmashauri Kuu na aliungana na Membe kuaga licha ya awali kupewa nafasi kubwa ya kushinda baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuenguliwa na Kamati Kuu ya chama hicho Ijumaa usiku.
Hii ni mara ya kwanza kwa wanawake kufika hatua ya tatu bora katika mchakato

No comments:
Post a Comment