Chris Brown akitoka klabu kabla ya kugundua kuwa nyumba yake imevamiwa.
TAARIFA kutoka vyombo vya usalama nchini Marekani zinaeleza kuwa
mwanamuziki Chris Brown alikuwa anafuatiliwa na watu kabla ya nyumba
yake iliyopo San Fernando Valley, Los Angeles, Marekani kuvamiwa na
majambazi jana.Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 8 usiku wakati mwanamuziki huyo akiwa katika Klabu ya Argyle iliyopo Hollywood, California.
Majambazi hao walivamia nyumba ya Chris na kumkuta shangazi yake ambapo walipora fedha na mali kadhaa kabla ya kutokomea.
Kuonyesha kuwa Chris alikuwa anafuatiliwa na watu hao, wanausalama wameeleza kuwa majambazi hao walimwambia shangazi wa Chris kuwa wanajua kuwa mwanamuziki huyo yupo klabu hivyo walifanya haraka ili waondoke kabla hajafika nyumbani hapo.
Chris anadaiwa kuwa na tabia ya kualika watu tofauti tofauti nyumbani kwake mara kadhaa atokapo klabu jambo ambalo linadaiwa kuwa linaweza kuwa sababu ya wizi huo.



No comments:
Post a Comment