AKIFUNGA bao lake la kwanza akiwa na Yanga,
mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Donald Ngoma, raia wa Zimbabwe, ametoa
kauli nzito ambayo inawahusu wapinzani wa Yanga lakini zaidi ni
wapinzani wa jadi wa timu hiyo, Simba.
Ngoma ambaye amekuwa gumzo tangu alipotua nchini hivi karibuni, juzi alifunga bao la kichwa katika mechi ya kirafiki dhidi ya KMKM kwenye Uwanja wa Taifa, jambo ambalo limeonekana kuwafurahisha mashabiki wa Yanga na kujiandaa kusubiri kumuona katika mechi za msimu ujao wa 2015/2016.
Aanza makeke
Ngoma ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, amejinadi kuwa bao alilofunga juzi akiunganisha kona iliyopigwa na Mbrazili, Andrey Coutinho ni mwanzo tu wa kile ambacho atakionyesha akiwa Yanga.
Awananga Simba
Straika huyo ambaye alishangilia kwa kuwaonyesha mashabiki wa Simba staili ya kuwataka watulie kwa kutumia mikono yake yote, ametoa maelezo juu ya kitendo chake hicho.
“Kabla ya mechi nilikuwa nimepewa taarifa juu ya ushabiki wa Simba na Yanga, hivyo niliingia kwa tahadhari kubwa.
“Kweli nilipoingia uwanjani nikaliona hilo, kwa kila tukio nililokuwa ninalifanya, wale mashabiki wa upande wa Simba wakawa wananizomea.
“Sikuwasikiliza, niliendelea na kazi yangu uwanjani, kwa sababu hali hiyo ya ushabiki ni ya kawaida ipo kila sehemu na ndiyo maana nilipofunga bao nikaenda kuwaambia kuwa watanyamaza kwa kutumia mikono yangu,” alisema Ngoma na kuongeza:
“Kipindi cha kwanza haikuwa rahisi kwani bado nilikuwa sijazoea mazingira ya mchezo ila kipindi cha pili nilikuwa sawa na wenzangu mpaka nikafanikiwa kufunga.”
Atengenezewa kombinesheni hatari
Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameonyesha kumkubali Ngoma na tayari ameanza kumfanyia mikakati ya kumtengenezea kombinesheni ya kumtumia pamoja na wenzake.Kocha huyo amekuwa akitafuta mbinu za kumtumia Ngoma pamoja na Mliberia, Kpah Sherman na Mrundi, Amiss Tambwe.
“Suala la kombinesheni ni jambo la kiufundi ambalo siwezi kulieleza kwa sasa, bado nalifanyia kazi,” alisema Pluijm na kuongeza:
“Ngoma alionekana kutokuwa sawa kipindi cha kwanza lakini uliona alichofanya kipindi cha pili? Hakuwa na mazoezi ya pamoja na timu kwa siku mbili kabla ya mechi hiyo lakini uzuri ni kwamba alijua afanye nini na hilo ndilo ninalolitaka.
“Ngoma ni mchezaji mzuri, watu wasubiri kuona mazuri tutakapoanza msimu, naamini atafanya vizuri tu, hilo sina wasiwasi nalo,” alisema Pluijm.
Niyonzima kutua leo
Wakati huohuo, kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima anatarajiwa kuwasili nchini leo akitokea kwao, Rwanda. Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema Niyonzima alichelewa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

No comments:
Post a Comment