TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza majimbo 26 mapya ya
uchaguzi ambayo yatakuwa na wagombea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika
Oktoba 25 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kukata kwa majimbo
hayo wamezingatia idadi ya watu pamoja na Jiografia katika majimbo
mapya.
Amesema katika upande wa Zanzibar majimbo yamebaki kuwa 50 kama awali hiyo inatokana vigezo vilivyowekwa na tume hiyo.
Majimbo yaliongezwa ni Handeni Mjini,
Nanyamba, Makambako, Butiama, Tarime Mjini, Tunduma, Msimbo, Kavu, Geita
Mjini, Mafinga Mjini, Ushetu, Nzega Mjini, Kahama Mjini, Kondoa Mjini,
Newala Mjini, Bunda Mjini, Mbulu Mjini, Ndanda, Madaba, Mbinga Mjini,
Mbagala, Kibamba,Vwawa,Monongo,Mlimba, Pamoja na Uliambulu.
Amesema baadhi majimbo yamebadilishwa majina na kuendelea kuwepo kwa majimbo hayo kisheria.
No comments:
Post a Comment