MZEE OJWANG AFARIKI DUNIA - LEKULE

Breaking

13 Jul 2015

MZEE OJWANG AFARIKI DUNIA

MWIGIZAJI nguli raia wa Kenya, Benson Wanjau 'Mzee Ojwang' amefariki dunia jana jioni akiwa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (Pneumonia).
Mzee Ojwang atakumbukwa katika Vipindi vya Televisheni kama Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na Kinyonga.

Amefariki akiwa na umri wa miaka 78.
Mzee Ojwang akiwa hospitali.

MAMBO 9 USIYOYAJUA KUHUSU MZEE OJWANG

1. Ojwang alizaliwa mwaka 1937 katika Wilaya ya Nyeri, Kenya.
2. Akiwa mwanafunzi wa Shule ya Msingi CMS, iliyopo Pumwani, Nairobi, Mzee Ojwang alikuwa akipendelea sana Somo la Hisabati.
3. Alilazimika kuacha shule akiwa kidato cha pili kutokana na matatizo ya kifedha.

4. Alimuoa Augusta Wanjiru na walibahatika kupata watoto wawili Patricia Njeri na Michael Karira.
zee Ojwang akiwa na Mama Kayai (Mary Khavere).

5. Familia ya Mzee Ojwang na Mama Kayai (Mary Khavere) ni marafiki wa karibu sana.
6. Mzee Ojwang alifanya kazi katika Hospitali ya Mater akiwa fundi.
7. Alianza kazi ya uigizaji mwaka 1980 kwenye Kipindi cha Darubini kilichokuwa kikiruka kwenye Kituo cha Voice of Kenya (sasa Shirika la Utangazaji la Kenya). Kipindi cha Darubini kilisitishwa mwaka 1985 baada ya Kipindi cha Vitimbi kuanza kuruka.
8. Mzee Ojwang hakuwahi kuzungumza lugha ya Kijaluo licha ya kuwa na lafudhi hiyo akiwa katika Vitimbi.

9. Jina lake la usanii 'Ojwang' lilitokana na rafiki yake wa karibu ambaye wakati akistaafu alimwambia kuwa asimsahau.

No comments: