
Bobby Brown akiwa na mkewe.
MWANAMUZIKI Bobby Brown amepata faraja baada ya mkewe Alicia Etheredge kumletea mtoto wa kike ambaye amejifungua hivi karibuni.
Wanandoa hao walioana mwaka 2012 ambapo walijaaliwa kupata watoto wa kiume ukiacha Bobbi Kristina ambaye ni wa Bobby Brown na sasa wamempata wa kike ambaye amewapoza machungu kutokana na Bobbi kuwa mgonjwa kwa muda mrefu.
Bobby Brown aliondokewa na amani ya moyo tangu Bobbi Kristina Brown apate kiharusi baada ya kuanguka chooni alikokutwa amepoteza fahamu.


No comments:
Post a Comment