MTOTO WA CIARA AGEUKA KIVUTIO - LEKULE

Breaking

20 Jul 2015

MTOTO WA CIARA AGEUKA KIVUTIO

CIARA AKIWA NA MWANAE

California, Marekani
MSANII wa R&B, Ciara Princess Harris hivi karibuni mtoto wake, Future Zahir aligeuka kivutio kwenye tamasha la utoaji tuzo za michezo ambazo huandaliwa na watoto ziitwazo, Kid’s Sports Choice Awards.

Katika tuzo hizo ambazo huandaliwa na Kituo cha TV cha Nickelodeon, Ciara alikuwa ameongozana na Future Zahir pamoja na mchumba wake, Rusell Wilson ambapo katika eneo la upigaji picha muda wote watoto walikuwa wakimshangaa mtoto wake.

Ciara aliyewahi kutamba na nyimbo nyingi ikiwemo 1, 2 Steps amewahi kutoka kimapenzi na wasanii kama Bow Wow, 50 Cent, mchezaji wa mpira wa kikapu Amar Stoudemire, rapa Future ambaye ndiye baba wa mtoto wake na sasa anatoka na Rusell.





No comments: