Bingwa wa michuano ya Olympic ya mwaka 2012, Mohamed “Mo” Farah,
ameonyesha ujasiri wa kupambana katika michuano ya Diamond League na
kufanikiwa kushinda mbio za mita 5,000 usiku wa kuamkia hii leo.
Farah, alikua anarejea uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kukumbwa na kashfa ya matumizi ya dawa za kusisimua misuhi, tuhuma ambazo alizipigania kwa kuzikanusha na hatimae alifanikiwa.
Mwanariadha huyo kutoka nchini England, aliyekua nje ya ushindani wa mchezo wa riadha tangu Juni mosi mwaka huu, alimaliza mbio hizo akiwa mkakamavu akifuatiwa na mwanariadha kutoka nchini Ethiopia, Yomif Kejelcha.
Farah, alitumia muda wa dakika 13, sekunde 11 na alama 77 huku mpinzani wake Kejelcha akitumia muda wa dakika 13, sekunde12 na alama 59 na Edwin Cheruiyot Soi kutoka nchini Kenya alishika nafasi ya tatu kwa kutumia dakika 13 sekunde 17 na alama 17.
Mara baadaya kuibuka mshindi katika mbio za mita 5000, Farah ambaye ni mzaliwa wa nchini Somalia, alizungumza na wanahabari na kuelezea furaha yake kwa kusema, ni bahati ilioje kwake kushinda hasa ikizingatiwa ametoka katika ombwe kubwa ambalo lilitaka kumpoteza katika tasnia ya mchezo wa riadha duniani.
Amesema alijitahidi kupambana kwa kujua wapinzani wake ni wazuri zaidi, lakini juhudi na maarifa aliyoyatumia yalikua chagizo kubwa la ushindi alioupata, ambapo anaamini umefungua njia ya kuendelea kujiandaa vyema zaidi kabla ya michuano ya dunia ambayo itafanyika mjini Beijing nchini china mwezi ujao.
Michuano ya Diamond League kwa jana ilifanyika Lausanne, nchini Uswiz.

No comments:
Post a Comment