Wiki kadhaa rapa Earl Simons a/k/a DMX
alitupwa selo huku akisubiri hukumu ya mahakama juu ya kesi
zilizomkabili ikiwezo ile ya kushindwa kulipa fedha ya matumizi kwa
mtoto wake pamoja na uvunjifu wa sheria za barabarani.
Kituo cha habari cha WIVB kimeripoti
kuwa, hakimu wa kesi za kifamilia Deanne Trippi ameshatoa hukumu yake na
kuanzia jana rapa huyo anatumikia kifungo cha miezi sita gerezani.
Habari hiyo inaonekana kumsikitisha
Mwanamuziki Shagy ambaye alishapanga kuwa na DMX mwaka huu kwenye
tamasha lake lijulikanalo kwa jina la Shaggfest.
Shaggy aliandika kwenye akaunt yake ya
mtandao wa twita, “ It comes with sadness and regret. But Dmx will not
be attending this year #shaggfest. — he got locked up today for 6
months.”
No comments:
Post a Comment