Mtia
nia kwa nafasi ya ubunge jimbo jipya la Kibamba kupitia tiketi ya CCM,
Bw.Stanslaus Justine Maganga (26) (Pichani) ametangaza kuwania nafasi ya
ubunge katika jimbo hilo.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe Dr. Fenella Ephrahim
Mukangara nae pia ni moja kati ya makada wa chama cha mapinduzi(ccm)
wanaothubutu kutia nia kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Kibamba
kupitia chama hiko.
Hali
ya kisiasa jimboni humo imepamba moto baada ya watia nia hao wawili
kuimarisha ngome zao kwa kupanga safu makini huku kila mmoja akijiwekea
mikakati ya kumbwaga mwenzie katika kura ya maoni inayotarajiwa
kufanyika hivi punde.
Kwa
habari za utafiti toka kibamba zinasema kuwa Bw. Maganga ambae ni mkazi
halisi wa eneo hilo kuwa anakubalika zaidi hasa kwa vijana na wamama
kutokana na kazi alizozozifanya kama kada wa chama na uwajibikaji wake
katika shughuli za kuleta maendeleo jimboni humo.
Aidha
aliongea kuwa alipata msukumo wa kutia nia baada kuona mapungufu katika
utendaji,ubunifu,uadilifu na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo
jimboni humo,ikiwemo miradi ya afya,maji na miundo mbinu.
Bw.Maganga
amesema kuwa endapo atapita katika kura za maoni na anaamini atashinda
ubunge hivyo atapeperusha vema bendera ya ccm na kutekeleza ilani ya
chama cha mapinduzi kwa nia kuu ya kuleta maendeleo kwa wananchi.
Kada
huyu ambae ana shahada ya kwanza katika biashara na uhasibu aliyoipata
katika chuo kikuu cha KIU,katika maswala ya uongozi aliwahi kuwa Makamu
wa Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, muasisi na Raisi wa
taasasi ya kupambana na rushwa vyuo vikuu (Interuniversity
anticorruption Associasion).
Pia
amewahi kuwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa Hondogo kata ya
kibamba,mjumbe wa baraza la katiba akiwakilisha vijanakataya
kibamba,mjumbe wa mkutano mkuu(ccm) kata ya kibamba.
Kwa
sasa Maganga ni mjumbe wa halmashauri kuu ya tawi la CCM maendeleo mtaa
wa Hondogo kibamba na mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM kata ya
kibamba.
Mwisho
alimalizia kwa kusema endapo akichaguliwa na kushika nafasi ya ubunge
ataenda kukomesha tatizo sugu la dhuluma za mashamba na ardhi ya raia
maskini dhidi wajanja wachache wanaonufaika isivyo halali.
Wakazi wa jimbo la kibamba wakimsikiliza mtia nia Bw.Stanslaus Justine Maganga wakati wa kutangaza nia.




No comments:
Post a Comment