KAMPUNI YA CHINA YAWEKA MASHARTI YA MTU KUPATA MIMBA - LEKULE

Breaking

3 Jul 2015

KAMPUNI YA CHINA YAWEKA MASHARTI YA MTU KUPATA MIMBA

KAMPUNI moja nchini China imepanga masharti kwa wafanyakazi wake wa kike ikiwa watataka kupata mimba.
Masharti hayo ambayo yamewekwa katika sheria za kampuni hiyo zimezua malalamiko mengi katika mitandao ambapo wanawake wote walio kwenye ndoa lazima wawe wamefanya kazi kwa mwaka mmoja kwenye kampuni hiyo kabla ya kutoa maombi ya kukubaliwa kushika mimba.
Kwa mujibu wa masharti hayo, anayekiuka utaratibu huo  na kushika mimba bila ya idhini, atatozwa faini au hapandishwi cheo.
Shirika la utangazaji la China limekosoa vikali kampuni hiyo iliyoko mkoa wa Henan na kusema haina ubinadamu kwa wafanyakazi wake.

Miongoni mwa masharti yanayoingilia uhuru binafsi wa watu nchini  China ni sheria ya familia kuzaa mtoto mmoja tu, sheria iliyowekwa na serikali miaka ya sabini.

No comments: