New
Naseeb ‘Diamond’ Plutnumz, ameridhia kwa mashabiki kuutumia msemo
aliouanzisha mara tu baada ya kushinda tuzo South Africa wa ‘mtanyooka
tu’.
Akichezesha taya na ripota wa Timesfm.co.tz, Chibu amefunguka kuwa
sentensi hiyo ina lengo la kumpa faraja muangaikaji yoyote kutokukata
tamaa katika ‘mishe’.
“Unajua sikuwa namaanisha vibaya, ilikuwa tu ni katika kujipa faraja
kwamba naweza fanya chochote kwa usahihi bila kuzuiwa na chochote”
alisema Plutnumz.
Katika line nyingine mkali huyo, yupo katika harakati za ‘kusuka’ mipango kukamilisha ‘collabo’ yake na mnyamwezi wa RNB Neyo.

No comments:
Post a Comment