Daktari feki akamatwa, aliihudumia hospital kwa miaka 9. - LEKULE

Breaking

8 Jul 2015

Daktari feki akamatwa, aliihudumia hospital kwa miaka 9.

Polisi mjini Abuja Nigeria, wanamshikilia bwana Martin Ugwu kwa kosa la kujifanya daktari katika hospital kuu mjini humo kwa miaka 9.
Mtandao wa Naijagists.com umeripoti kuwa, Martin alikuwa akitumia kadi ya rafiki yake ambaye ni kiongozi hospitalini hapo kuingia wodini na ofisi mbali mbali.

Kwenye “line” nyingine mshtakiwa huyo amekiri tukio hilo, huku akidai aliamua kufanya hivyo kwa kile alichoeleza upungufu wa madaktari hospitalini hapo.

No comments: