Mshambuliaji wa klabu ya Fluminense, Robert Kenedy Nunes do
Nascimento jana jioni alifanyiwa vipimo vya afya huko jijini London,
ikiwa ni sehemu ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu bingwa
nchini England, Chelsea kwa ada ya uhamisho wa paund million 6.3.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, alikua kwenye mipango ya kuelekea jijini London kukamilisha uhamisho wake tangu majuma mawili yaliyopita baada ya viongozi wa klabu ya Fluminense kumaliza mazungumzo na viongozi wa Chelsea.
Kenedy atakuwa mchezaji wa pili kusajili huko Stamford Bridge akitokea nchini Brazil kwa mwaka huu, baada ya usajili wa Nathan aliyekua akiitumikia klabu ya Atletico Paranaense mwezi May.
Hata hivyo Kenedy alikua akifuatiliwa kwa ukaribu na klabu kubwa barani Ulaya kama Manchester United, Barcelona, Juventus pamoja na Wolfsburg ya nchini Ujerumani, lakini Chelsea wametumia mbinu zao na kufanikiwa kumnasa kwa urahisi.
Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa wachezaji wanaocheza katika kikosi cha timu ya taifa ya Brazil chini ya umri wa miaka 20.

No comments:
Post a Comment