Dar es Salaam.
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia kwa makini uandikishaji wapigakura jijini hapa ili wakazi wote wapate fursa ya kuandikishwa, ndani ya muda uliopangwa.
Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia kwa makini uandikishaji wapigakura jijini hapa ili wakazi wote wapate fursa ya kuandikishwa, ndani ya muda uliopangwa.
Katibu wa
Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba
aliwaambia wanahabari jana kuwa ufanisi katika uandikishaji utasaidia
kumaliza idadi kubwa ya wakazi ambao bado hawajaandikishwa hadi sasa.
“NEC
inatakiwa kuwa makini kukamilisha uandikishaji kwa kuongeza mashine na
watendaji ili wakazi wengi wa Dar es Salaam waandikishwe,” alisema.
Kuhusu Lowassa
Simba alisema CCM haitatetereka na uamuzi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia Chadema.
Alisema uamuzi huo siyo wa kwanza, kwani Augustine Mrema aliwahi kuondoka CCM na kujiunga na upinzani.
Alisema uamuzi huo siyo wa kwanza, kwani Augustine Mrema aliwahi kuondoka CCM na kujiunga na upinzani.
Kauli
ya kiongozi huyo imekuja siku moja tangu Lowassa na mkewe, Regina,
waihame CCM na kujiunga na Chadema na kuahidi kuendelea na safari ya
matumaini ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
“Lowassa
alijiunga CCM kwa ridhaa yake, hakuna aliyemshurutisha na ametoka kwa
ridhaa yake kwenda Chadema hakuna aliyemshurutisha. “CCM itabaki kuwa
CCM zaidi ya hilo, lipi jipya?”
Simba alisema tishio kwamba Lowassa ataondoka na makada wengi wa chama hicho ni propaganda za kupuuzwa.
Jaji Lubuva alonga
Akizungumza
na mwandishi wetu jana, Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva
alisema muda wa kuandikisha wapigakura utaongezwa baada ya kujua idadi
ya watakaosalia ifikapo mwisho wa kujiandikisha Agosti 31.
“Kwa
sasa hatuwezi kusema tutaongeza siku ngapi, lakini ikifika siku ya
mwisho tutajua watu wangapi wamebaki na hapo ndipo tutaongeza muda au
la,” alisema Lubuva.
Alisema utaratibu wa kuanza
uandikishaji kuanzia saa moja asubuhi hadi 12 jioni, unaweza kuongeza
kasi ya uandikishaji na hivyo watakaosalia watapewa muda kulingana na
idadi yao.
Waandikishaji wakaidi agizo la NEC
Licha
ya NEC kutoa agizo kwa mawakala wa BVR kuanza kufungua vituo kuanzia
saa moja asubuhi, badala ya saa mbili, baadhi ya mawakala katika vituo
wamekaidi agizo hilo.
Jaji Lubuva alitoa agizo hilo
juzi akiwataka mawakala hao kufungua vituo muda huo lengo likiwa
kuhakikisha idadi kubwa ya watu wanaandikishwa.
Hata
hivyo, agizo hilo lilionekana kupuuzwa na mawakala wa baadhi ya vituo
ambao walifungua vituo hivyo kati ya saa mbili na saa tatu asubuhi.
Waandishi
wetu walipita katika baadhi ya vituo na kukuta watu wakilalamikia suala
hilo. Mmoja wa wananchi waliokuwa kwenye Kituo cha Shule ya Msingi
Mivinjeni, Lekule Mollel alisema walifika kituoni hapo mapema, lakini
kilifunguliwa saa tatu asubuhi na siyo saa moja kama inavyotakiwa.
Wakala
wa kituo hicho, Malick Shaaban alikiri kuchelewa kufunguliwa kwa kituo
hicho na kudai kuwa baadhi ya mawakala wanaishi mbali na eneo hilo.
Katika vituo vya Tabata, Temeke na Mbagala wananchi pia wamelalamik baadhi ya vituo kuchelewewa kufunguliwa tofauti na agizo.
Mkazi
wa Tabata, aliyekuwa akijiandikisha kwenye Kituo cha Shule ya Sekondari
Ari B, Tabata Kinyerezi, Elizabeth Mwijage alisema baadhi ya mawakala
wa kituo hicho walipoulizwa juu ya hilo walidai hawakuwa na taarifa.
Licha
ya kwamba walifungua saa moja, lakini uandikishaji ulianza saa tatu
asubuhi kutokana na matatizo ya mashine kugoma kabla ya kuanza kazi.
“Tumefika
hapa saa kumi na moja alfajiri tulivyoona wamewahi kufungua kituo
tulifurahi tukijua uandikishaji utaanza mapema, lakini mashine
zilichukua muda ilipofika saa tatu ndiyo mtu wa kwanza alianza
kuandikishwa,” alisema Juma Pascal aliyekuwa Kituo cha Serikali ya Mtaa
Kibondemaji B.
No comments:
Post a Comment