Breaking News kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar kuhusu Silaha zilizoibiwa Kituo cha Polisi Stakishari.. - LEKULE

Breaking

20 Jul 2015

Breaking News kutoka Makao Makuu ya Polisi Dar kuhusu Silaha zilizoibiwa Kituo cha Polisi Stakishari..


Kwenye mfululizo wa matukio yaliyoshtua watu wengi Tanzania, liko pia ambalo lilitokea usiku wa July 12 2015 ambapo Majambazi walivamia Kituo cha Polisi Stakishari Ukonga Dar, wakauawa watu 7 wakiwemo pia Askari wanne na watu wengine watatu.
Leo taarifa imetolewa na Kamanda Suleiman Kova kwamba kuna watu watano wamekamatwa wakihusishwa na tukio hilo na pia kuna silaha ambazo zimekamatwa, ziko Bunduki 15 pamoja na Risasi 28 ambazo zote ni sehemu ya zilizoibiwa wakati wa tukio la Ujambazi uliofanyika Stakishari.


No comments: