Blatter atupiwa pesa Zurich - LEKULE

Breaking

22 Jul 2015

Blatter atupiwa pesa Zurich


Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ametupiwa pesa na mtu aliyevamia mkutano wake na wanahabari.
Mvamizi huyo aliyetambuliwa kama Lee Nelson raia wa Uingereza aliondolewa ukumbini humo mara moja na maafisa wa usalama wa FIFA.
Blatter aliyekuwa ameudhika sana na tukio hilo alisema 'halikuhusiana kwa njia yeyote na kandanda' kabla yake kuondoka ukumbini.
Blatter alitangaza mabadiliko kadha ikianza na tarehe ya uchaguzi ambayo itakuwa mwezi Februari mwakani.

Aidha Viongozi watakaokuwa na ari ya kurithi kiti hicho cha rais wa FIFA,sharti wawasilishe rasmi maombi yao kabla ya tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu.
Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) Michel Platini, anadaiwa kupata shinikizo kutoka kwa viongozi wengi wa bara hilo kuwasilisha ombi lake la kuwa rais wa FIFA.
Mkutano huo wa leo pia ulitaja baadhi ya mambo yatakayorekebishwa ikiwa ni pamoja na kuweka kikomo cha muhula cha urais na viongozi wengine wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo.

Hatua ya kuchapisha mishahara na marupurupu ya viongozi wa ngazi ya juu wa shirikisho hilo pia ilijadiliwa.
Aidha FIFA itateua jopo la watu 11 watakaoanza uchunguzi wa kina kubaini njia za kukabiliana na rushwa na ubadhirifu.
Jopo hilo maalum ndilo litakaloendesha mabadiliko katika Fifa.

No comments: