Bi Hindu Awa kiongozi Simba - LEKULE

Breaking

6 Jul 2015

Bi Hindu Awa kiongozi Simba

Mtangazaji wa 100.5 Times fm Bi Chuma Suleimani a/k/a Bi Hindu ameteuliwa kuwa Mwanamke pekee katika Baraza jipya la wazee la klabu ya wekundu wa msimbazi Simba SC lililotangazwa na kamati ya utendaji ya Simba.
Bi Hindu anaungana na wazee wengine wa kipindi tangu Simba inaitwa Sunderland, Omary Mtika (Mwenyekiti), Ally Hassan, Abdulsharif Zahoro na Omary Moshi.
Akizungumzia uteuzi huo Bi Hindu ambaye husikika kila siku za Jumatatu – Alhamis saa sita mchana mpaka saa kumi kwenye kipindi cha Mitikisiko ya pwani (Timesfm), amesema kuwa amefurahia uteuzi huo na ameahidi kuendelea kujitolea kwa mapenzi yake yote kuijenga klabu hiyo.
“Aveva ana busara na akili ameona haitowezekana kuendesha jambo peke yao bila ya wakongwe ambao wapo ndio kama sisi tuloitumikia kitambo, nawapongeza sana Mwenyezi Mungu awabariki sana na nafurahi sana lakini kubwa akili zao nafuu zao na raha yangu mimi Tukutane Oktoba”, alisema Bi Hindu.
Uteuzi wa Bi Hindu pamoja na wazee wengine umekuja mwaka mmoja tangu uongozi mpya wa Simba chini ya Rais Evans Elieza Aveva uingie madarakani mwezi june mwaka 2014.

Hongera sana Bi Chuma Suleiman Bi Hindi Bibi wa Mcharazo wa Bi Mkubwa kwa hatua hiyo.

No comments: