Belle 9 amedai kuwa kwenye muziki wake haamini kama collabo ni njia sahihi ya kumfikisha kimataifa zaidi.
Akizungumza na mtandao huu, Belle amesema wapo wasanii kadhaa walioweza
kutoboa bila hata kufanya collabo na wasanii wa mataifa ya nje.
“Mimi nimefanya collabo na Joh Makini, I am proud kwa sababu ni
msanii mkubwa ambaye anafanya vizuri ndani na nje. Joh is too expensive
sio simple tu kufanya naye collabo,” amesema Belle.
“Kama unavyojua msanii mkali hawezi kurekodi na msanii mbovu, mimi
naamini inawezekana. Mimi naamini collabo sio kitu kinawezeka
kunifikisha International, sijui wasanii wenzangu wengine.
"Kwa sababu
mtu kama Gsan alishiriki mpaka cipher ya BET najua sio kawaida, sasa
Gsan alifanya collabo na nani? Na ni washkaji ambao walikuwa level
kubwa.
"Mimi siamini collabo inaweza kunifikisha huko, yaani siamini
katika collabo kwa sababu ningekuwa nimeshafanya na nimesharelease.
"Lakini najua collabo ni maisha ya muziki ambayo inatokea ukafanya lakini
mimi sijafikiria nijaribu kufanya ndio nifike huko,” aliongeza muimbaji
huyo.
Belle anajiandaa kuachia video ya wimbo wake ‘Shauri Zao’ iliyoongozwa na Hanscana.
No comments:
Post a Comment