Msanii wa filamu nchini, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli amesema
mashabiki wake wa filamu wasione yupo kimya kwakuwa yupo kwenye mpango
kuthubutu kama alivyothubutu marehemu Steven Kanumba kwa kuaanda filamu
itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni 40.
Batuli ameuambia mtandao huu kuwa licha ya kuwa anafanya filamu
zilizozoeleka, anajipanga kufanya kitu kikubwa ili kuipa heshima tasnia
ya filamu nchini Tanzania.
“Kazi zangu zinaenda bomba lakini kuna kazi ambazo zinahitaji udhamin
Kwa sababu ni kazi tofauti na hizi zilizozoeleka.Inahitaji watu wengi,
kazi inayohitaji milioni 40 na kuendelea. Kwahiyo tunahitaji udhamini
kwa sababu ni tofauti na filamu hizo ambazo tumezizoea,” amesema
muigizaji huyo.
“Ni filamu ambayo ipo kijamii zaidi, imezama ndani zaidi, yaAni
nafanya kitu kikubwa bila kujua nitapata nini. Nataka kuthubutu kama
alivyothubutu Kanumba na ndo maana nipo cool nahangaikia udhamini ili
nikamilishe hili.
"Mpaka sasa hivi huu ni mwezi wa 5 nipo kwenye
maandalizi na bado naona itafika mpaka mwezi wa 12, kwahiyo wadau
wasubirie. Ila pia kuna kazi filamu hizi za kawaida zitaendelea kutoka,”
ameongeza Batuli.
Katika hatua ngingine Batuli amewapongeza wasanii waliojitokeza
kugombea nyadhifa mbalimbali za siasa huku yeye akitoa sababu ya kukaa
pembeni kwa wakati huu.
“Mimi nitatangaza nia yangu wakati ukishafika, inawezekana labda kuna
kitu nakitaka labda sio uwaziri labda ni kitu fulani ambacho kinafanana
na kitu kama hicho.
"Pia nawapongeza wote waliotangaza nia, wameonyesha
kujiamini.
"Pia naomba wawapokee wasanii wenzangu sio wote ila wale ambao
wanawaona wanafaa kwa sababu sio wote wanafaa hata kwenye watu kumi
kuna wa kwanza mpaka wa kumi. Kwahiyo wawapokee wasanii wenzangu kwenye
siasa.”
No comments:
Post a Comment