Watu wanne wamefariki papo hapo na wengine zaidi ya arobaini
kujeruhiwa baada ya Treini ya mizigo,kuligonga basi kampuni ya Don’t
Worry lililokuwa likitokea mjiniTabora kuelekea ufuruma uyui mkoani
humo lilipofika eneo la kuvuko cha reli eneo loa malolo manispaa ya
Tabora katika kile kilichodaiwa kuwa ni uzembe wa dereva.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa, dereva aliyekuwa katika
mwendo wa kasi alitaka kukatiza haraka bila kuzingatia eneo hilo
inapopita Treini hata kama aliiona Treini hiyo, na ndipo alipokata kona
ya ghafla na basi hilo kuanguka kwenye reli na Treini kuigonga na
kukutoa paa lote la juu la gari.
Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi
Juma Bwire amesema kuwa katika ajali hiyo ya basi lenye namba za usajili
T568 ABP,wanaume watatu na mwanamke mmoja wamepoteza maisha huku dereva
aliyejulikana kwa jina la Kaonjo Iddy (34) akitoroka baada ya
kusababisha ajali hiyo ambapo majeruhu wamepelekwa katika hospitali ya
rufaa na mkoa wa Tabora.
Viongozi wa shirika la reli waliofika katika eneo la ajali hiyo
wamesema kuwa madereva hawazingatii usalama wa barabarani kwani shirika
la reli limejitahidi kuhakikisha linaweka alama husika lakini kutokana
na mazoea mabaya hawajali na matokeo ni kusababisha ajali mbaya kama
hiyo.




No comments:
Post a Comment