Shirika la Umoja wa Mataifa
linalosimamia chakula WFP limesema kuwa litapunguza kiwango cha chakula
kwa takriban wakimbizi nusu milioni kazkazini mwa Kenya kutokana na
ukosefu wa ufadhili.
WFP limesema kuwa litapunguza chakula hicho
kwa thuluthi moja katika kambi mbili za Dadaab na Kakuma ambazo ni
makaazi ya wakimbizi kutoka Somalia na Sudan Kusini.Pia limeomba ufadhili wa dola milioni 12.
Mnamo mwezi Novemba mwaka uliopita shirika hilo lililazimika kupunguza hadi nusu kiwango cha chakula huku likisubiri kupata ufadhili zaidi.
No comments:
Post a Comment