WAKILI
wa kujitegemea Yasinter Rechungura (45), ametoa ushahidi Mahakamani na
kudai kwamba aliyekuwa mfanyakazi wake wa ndani Merina Mathayo (16),
hakuwahi kumpiga wala kumjeruhi badala yake alijeruhiwa wakati akichota
maji katika SIMTANK lililopo nyumbani kwake Boko Magengani.
Yasinter
alitoa ushahidi huo jana Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam
mbele ya Hakimu Amalia Mushi, na Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Masini
Musa wakati Wakili wa utetezi Benitho Mandele.
Alidai
kuwa Merina siku moja wakiwa nyumbani Merina alienda kuchota maji
katika simtank lililopo kando ya nyumba ndipo aliteleza na kuanguka juu
ya sehemu iliyokuwa na vigae, mawe, mbao, matofali na kuumia kichwani na
sehemu nyingine.
“Mheshimiwa
mimi mwenyewe nilishangaa kama mzazi kwa kuwa Merina baada ya kurudi
kuchota maji alikuwa anavuja damu nyingi sehemu za usomi ila baada ya
kumwuliza hakunipa jibu sahihi ili nilihisi alianguka kwenye hilo tanki
la maji kwa kuwa nilipokuwa ndani nilisikia kishindo.
“Baada
ya kuona hali ile kwanza nilichanganyikiwa kisha nikawapigia simu
wadogo zangu Flora na Josephine waje wanisaidie kumpeleka Hospitali
kwani mimi nilikuwa nina mtoto mdogo ambaye naye hali yake ki afya
haikuwa njema,” alidai Yasinter.
Awali
aliiambia Mahakama hiyo kwamba Merina alipokuja nyumbani kwake kutoka
Bukoba alikuwa anaonekana akiwa na alama za makovu kichwani kwake na
baada ya siku kadhaa alipomwuliza alimwambia kwamba yalisababishwa na
kupigwa na baba yake wakati mengine aliumia akicheza na wenzake.
Aidha,
kwa maelezo hayo wakili huyo aliiomba mahakama iangalie suala hilo kwa
kina kisha imfutie shauri hilo na kumwachia huru kwani hakutenda kosa
hilo kwa kuwa yeye pia ni mzazi mwenye watoto kama Merina.
Shahidi
wa pili wa utetezi Josephine Rwechungura (48), alidai kuwa wakati
akiendelea kumtibu Merina katika Hospitali ya Mwananyamala alishangaa
umati wa watu ukimvamia na kuanza kumhoji kwamba ni kwa nini anataka
kuua mtoto?
“Mheshimiwa
nikiwa Haspitali ya Mwnanyamala walikuwa Waandishi wa habari,
Wanaharakati, watu kutoka Kituo cha Sheria na haki za binadamu LHRC
pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),
wakiwa na polisi wakaanza kuni hoji.
“Niliambiwa
kuwa mimi ni mtesaji, muuaji kitu ambacho ni uongo kwa kweli niliishiwa
nguvu kwani nilikuwa namletea mgonjwa chakula,” alidai Josephine.
Alilaani
kitendo cha askari wa kituo cha Polisi Kawe baada ya kumkamata
alilazimishwa kutia saini maelezo ambayo tayari yalikuwa yameandikwa
bila kupewa muda wa kuyasoma wala kusomewa kosa lake.
No comments:
Post a Comment