Urais 2015: Mwigulu achukua fomu,Asema Kikwete ni Rais wa Mwisho Kutawala Tanzania Masikini - LEKULE

Breaking

6 Jun 2015

Urais 2015: Mwigulu achukua fomu,Asema Kikwete ni Rais wa Mwisho Kutawala Tanzania Masikini


Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba pamoja na Mke wake katika ukumbi wa makao makuu ya CCM Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba akiongea na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa NEC Dodoma.

Mke wa Mwigulu Nchemba akiwasalimia Waandishi wa Habari.

Naibu waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba katika mkutano na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais leo

Naibu Waziri waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba leo amechukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiwa atateuliwa na chama chake cha Mapinduzi kupeperusha bendera ya Tanzania katika uchagauzi mkuu ujao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari amesema kwamba atahakikisha anaboresha uchumi kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kuboresha njia kuu za wananchi kupata kipato. Kufufua viwanda vilivyokufa ili kutoa ajira kwa vijana pamoja na kudhibiti madawa ya Kulevya, Rushwa na ufisadi.

Amesisitiza kuwa Rais Kikwete ndiye rais wa mwisho kutawala Tanzania maskini.

No comments: