Rais wa Gambia aongezewa jina jingine - LEKULE

Breaking

18 Jun 2015

Rais wa Gambia aongezewa jina jingine

Rais wa taifa la Gambia ambaye amekaa kwa kipindi kirefu madarakani Yahya Jammeh ameongezwa jina la Babili Mansa juu ya jina lake.
Kulingana na kabila la Mandika jina hilo lina maana ya 'mtengezaji daraja mkuu' ama 'mshindi wa mito'.
Taarifa kutoka kwa rais imesema kuwa rais Jammeh sasa anapaswa kuitwa mtukufu Sheikh Profesa Alhaji daktari Yahya AJJ Jammeh Babili Mansa.
Alichukua jina hilo mara moja mwaka 2014 kabla kuliacha kulingana na ripoti.
Rais Jammeh alichukua mamlaka mwaka 1994 alipokuwa luteni wa jeshi na amefanikiwa kushinda chaguzi 4 ambazo zimekosolewa mbali na kukabiliwa na majaribio kadhaa ya mapinduzi.
Ameiambia BBC mwaka 2011 kwamba atatawala kwa miaka bilioni moja..iwapo Mungu atamruhusu.
Iwapo ungependa kuongeza jina jingine juu ya jina lako basi ni jina gani ungependelea kupewa?

No comments: