Mwanaharakati anayejifanya mtu mweusi - LEKULE

Breaking

13 Jun 2015

Mwanaharakati anayejifanya mtu mweusi

Wazazi wa mwanaharakati mmoja wa haki za raia nchini Marekani wamesema kuwa anajifanya kuwa mtu mweusi kwa miaka kadhaa sasa.
Rachel Dolezal analifanyia kazi shirika liitwalo National Association for the Advancement of Colored People {NAACP} huko Spokane takriban maili 280 mwa mji wa Seattle kazkazini magharibi mwa Marekani.
Kulingana na msemaji wa gazeti la Review,Dolezal amesema kuwa yeye ni mchanganyiko wa mtu mweupe,mweusi na muhindi wa Marekani katika ombi lake alilowasilisha kwa tume ya polisi inayosimamia malalamishi ya raia mnamo mwezi Januari.
Ombi hilo sasa linachunguzwa.Meya wa mji wa Spokane David Condon na rais wa baraza la mji huo Ben Stuckart alitoa taarifa.
Kwa miaka mingi Rachel Dolezal anasema kuwa yeye ni mzaliwa mwenye mizizi ya Kiafrika na Marekani madai ambayo wazazi wake wamekana.Nilikutana na Rachel Dolezal na sikuwa na wasiwasi kuhusu anakotoka.
Wazazi wa Dolezal ambao ni wazungu Ruthanne na Lawrence wamesema kuwa ni mwana wao wa kumzaa.

No comments: