Mo Farah alikosa kufanyiwa ukaguzi 2010 - LEKULE

Breaking

18 Jun 2015

Mo Farah alikosa kufanyiwa ukaguzi 2010

Medali za dhahabu alizoshinda mwanariadha wa Uingereza Mo Farah huenda ndizo zilizotawala mbio za mwaka 2012 mjini London.Lakini sasa huenda dhahabu hizo zipo hatarini.
Kulingana na gazeti la Daily Mail,mwanariadha huyo wa Uingereza alikosa ukaguzi wa kimatibabu mwaka 2010 na mwengine mwaka uliofuatia.
Iwapo angekosa ukaguzi huo kwa mara ya tatu ndani ya kipindi cha miezi 18,Farah angekabiliwa na marufuku ya miaka minne na kukosa kushiriki katika mashindano ya Olimpiki.

Haya yote yanajiri kufuatia makala ndefu ya BBC wiki mbili zilizopita kwamba kocha wa mwanariadha huyo Alberto Salazar pamoja na mwenzake ambaye amekuwa akifanya mazoezi naye Galen Rupp walihusika na sakata ya madawa ya kusisimua misuli.
Wote wamekana kufanya makosa yoyote na hakuna maelezo yoyote kwamba Farah alikiuka sheria zozote.
Gazeti hilo linasema kuwa Mo Farah alikosa ukaguzi wake wa kwanza miezi kadhaa kabla kujiunga na kocha wake mjini Oregon mapema mwaka 2011.

Mara ya pili ilitokea,lakini mwanariadha huyo akaliomba shirika linalokabiliana na dawa za kusisimua misuli nchini Uingereza akielezea kwamba hakusikia kengele wakati maafisa wa shirika hilo walipomtembelea nyumbani kwake.
Farah kwa sasa anafanya mazoezi nchini Ufaransa baada ya kuthibitisha kwamba atashiriki katika mashindano ya mwezi ujao kwa mara ya kwanza tangu madai ya kutumia dawa za kusisimua misuli yatolewe dhidi ya kocha wake.

No comments: