Mauaji ya silaha za moto yaongezeka New York, US - LEKULE

Breaking

3 Jun 2015

Mauaji ya silaha za moto yaongezeka New York, US


Ripoti zinaeleza kuwa matukio ya utumiaji silaha za moto mjini New York, Marekani yameongezeka kwa mwaka wa pili mtawalia. Idara ya polisi ya mji huo imetangaza kuwa, mwaka huu pekee wa 2015 watu 439 wamekwishapoteza maisha hadi sasa kutokana na vitendo vya ukatili na utumiaji silaha hizo za moto, kiasi kinachotajwa kuwa ni ongezeko la asilimia tisa zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita wa 2014. JamesP. O'Neill, mkuu wa polisi ya mji wa New York amenukuliwa akisema kuwa, ufyatuaji risasi na mauaji yatokanayo na utumiaji wa silaha za moto ni moja ya matatizo makubwa yanayoukabili mji huo hivi sasa. Kwa mujibu wa O'Neill, mwaka huu pekee jumla ya watu 135 wameuawa mjini hapo kwa kupigwa risasi, suala ambalo linawafanya wakazi wa mji huo kuishi katika hali ya kutoaminiana. Ni vyema ifahamike kuwa, vitendo vya utumiaji silaha za moto vimeshika kasi zaidi si mjini New York pekee, bali ndani ya Marekani kwa ujumla na inaelezwa kuwa, kwa kila mwaka zaidi ya watu elfu 11 hupoteza maisha nchini humo, kutokana na matumizi ya silaha hizo. Kufuatia hali hiyo, ndipo Rais Barack Obama wa nchi hiyo akatakiwa kutia saini muswada wa kuchunguza upya umiliki wa silaha za moto ndani ya taifa hilo, pendekezo ambalo hadi sasa limeendelea kupuuzwa na rais huyo.





No comments: