Marekani yahamisha 6 kutoka Guantanamo - LEKULE

Breaking

13 Jun 2015

Marekani yahamisha 6 kutoka Guantanamo

Marekani inasema kuwa imewaamisha wafungwa sita raia wa Yemen waliokuwa wamezuiliwa kwa miaka mingi katika gereza la Guantanamo kwenda nchini Oman.
Makao makuu ya jeshi la Marekani yametoa shukran kwa taifa hilo la ghuba katika kile yamesema kuwa ni ishara ya ubinadamu.



Yameishukuru Oman kwa kujitolea kuunga mkono jitihada za marekani za kufunga gereza la Guatanamo.
Rais Obama alikuwa ameahidi kufunga gereza la Guantanamo wakati akifanya kampeni mwaka 2008 lakini hajafanya hivyo.
Hata hivyo utawala wake umepunguza idadi ya wafungwa kwa nusu






No comments: