Imeripotiwa kuwa Raisi wa Fifa,Sepp Blatter anafanyiwa uchunguzi na maafisa wa marekani ili kuthibitisha tuhuma ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA.
Taarifa hiyo inakuja baada ya Blatter kutangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.
Wakati ambao waendesha mashtaka nchini Marekani wanaoifuatilia tuhuma za rushwa walikamata maafisa saba wa Fifa nchini Switzerland kati ya watu 14 wanaotuhumiwa kwenye kashfa hiyo.
Hata hivyo Blatter alisema anatumia mamlaka aliyopewa hata kama hayakubaliwi na kila mtu duniani.
Fifa inahitaji mabadiliko makubwa ili kukemea rushwa.
Mwandishi wa BBC,Nick Bryant mjini New York anasema kuwa bado maafisa hao wa marekani wana matumaini ya kupata ushirikiano kutoka kwenye takwimu za Fifa kwa sasa ili kubaini namna ambavyo mzunguko wa pesa chafu unavyomuhusisha Blatter.
Katika taarifa iliyoripotiwa kutoka kwa maafisa wa Marekani wiki iliyopita kuhusu rushwa katika shirikisho hilo la soka ulimwenguni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Loretta Lynch haikumshutumu Blatter moja kwa moja .
Ingawa alisema kuwa huu ni mwanzo tu wa uchunguzi na si mwisho.
Mwandishi wetu anasema huu ni msingi wa maafisa wa marekani katika kuikomboa dunia katika majanga makubwa kama haya.
Mwanzoni FBI,mamlaka ya ndani ya huduma za Mapato nchini Marekani na mwanasheria wa New York , ambaye alishiriki katika uchunguzi huo walisema kuwa hawana maoni juu ya kujiuzulu kwa Blatter.
No comments:
Post a Comment