Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana Aanza Ziara Mwanza Leo. - LEKULE

Breaking

21 Jun 2015

Katibu Mkuu wa CCM , Abdulrahman Kinana Aanza Ziara Mwanza Leo.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, leo anatarajia kuanza ziara ya siku kumi mkoani hapa, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kuimarisha uhai wa chama.
 
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa CCM Mkoa Mwanza, Miraji Mtaturu kwa waandishi wa habari, imeeleza kuwa Kinana ataanzia ziara yake katika Kijiji cha Nyamadoke, Wilaya ya Sengerema akitokea mkoani Geita.
 
“Ziara ya Katibu Mkuu Kinana akiwa mkoani Mwanza itakuwa ya kihistoria kwa sababu atafika kwenye baadhi ya maeneo ya wilaya za Ukerewe na Misungwi ambayo viongozi wa CCM kitaifa na Serikali hawajawahi kufika tangu kupatikana kwa uhuru wa taifa hili.
 
 “Ni lengo sisi kama chama kuitumia ziara hiyo kurejesha hamasa kwa wana CCM ili tuweze kuyarudisha majimbo ya ubunge yaliyochukuliwa na upinzani mwaka 2010,” alisema Mtaturu.
 
Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo Kinana atafika na kuwa kiongozi wa kwanza wa kitaifa wa CCM kuyatembelea kuwa ni Kisiwa cha Ilugwa kilichopo wilayani Ukerewe ambapo atashiriki ujenzi wa kituo cha afya na baadaye ataelekea Kijiji cha Mahando, wilayani Misungwi atakakoweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi ya CCM kabla ya kupokea wanachama wapya na kuwakabidhi kadi.
 

Mtaturu alizitaja wilaya ambazo Kinana atazitembelea kuwa ni Kwimba, Magu, Nyamagana, Ilemela na Ukerewe.

No comments: