Dodoma.
Kumekucha na Hapatoshi mjini Dodoma. Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo mjini hapa, wiki mbili kabla ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kazi ya kumtafuta mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Kumekucha na Hapatoshi mjini Dodoma. Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea hali ilivyo mjini hapa, wiki mbili kabla ya vikao vya juu vya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuanza kazi ya kumtafuta mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Hekaheka
za maandalizi ya vikao hivyo kuanzia vya maadili, Sekretarieti, Kamati
Kuu, Halmashauri Kuu ya Taifa na Mkutano Mkuu wa Taifa, zimeanza
kuonekana wazi huku nyumba zote za kulala wageni na hoteli zikiwa
zimekwishajaa kwa muda wote wa vikao hivyo.
Uchunguzi
uliofanywa na Mwananchi kwenye maeneo ya katikati ya mji wa Dodoma,
umebaini kuwa nyumba za kulala wageni na hoteli zimejaa kuanzia Julai 8
hadi 12, mwaka huu.
Hali hiyo imewafanya watu wanaotaka kupanga katika nyumba hizo kuulizwa wataondoka lini, ili tarehe za ‘booking’ zisigongane.
“Utaondoka
lini, maana CCM wamechukua nyumba zote hapa kati ya Julai 8 hadi 12,”
alisema mmoja wa wahudumu katika nyumba ya kulala wageni ya Kiramiya.
Chanzo
cha habari kutoka katika ofisi ya CCM, kimesema wajumbe wote 2,448 wa
mkutano mkuu wamepata maeneo ya kulala kwa siku watakazokuwa mjini hapa.
Hata
hivyo, chanzo hicho kimedokeza kuwa changamoto imekuwa katika kupata
malazi ya wageni 600 waalikwa, watakaokuja kuhudhuria mkutano mkuu huo
utakaofanyika katika ukumbi mpya wa chama hicho.
“Katika
maeneo mengi tuliyokwenda tulikuta hoteli zimechukuliwa na wapambe wa
wagombea wa urais ambao tayari wamelipia siku watakazokaa mjini hapa,”
alisema mmoja wa wanakamati ya maandalizi ya CCM na kuongeza:
“Hivi sasa wenzangu wako mtaani wanatafuta nyumba nyingine.”
Alisema
hali imekuwa ngumu kutokana na wapambe wa wagombea ambao hadi sasa
wamefikia 39 kuchukua vyumba vingi na kuvilipia kabisa, tofauti na CCM
iliyopanga kuanza kulipia malazi hayo leo.
Ukarabati
Katika
hatua nyingine, mafundi wameonekana wakifanya marekebisho katika
majengo ya makao makuu ya chama hicho hasa jengo maarufu la ‘White
House’ ulipo ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.
“Hujaingia
humo ndani lakini ukumbi unafanyiwa marekebisho makubwa ili mjumbe
atakayekaa mwisho aweze kuona mbele kwa urahisi, siyo kama ilivyokuwa
zamani,” alisema mmoja wa makada wa chama hicho.
Nje ya
ofisi hizo, wafanyabiashara wanaouza sare za chama hicho na bidhaa
nyingine za kumbukumbu za chama, wamekwishaanza kupanga biashara zao
kandokando ya ukuta wa jengo hilo wakisubiri kunufaika na wingi wa
wageni mjini hapa.
Jumla ya wagombea 39 wamejitokeza
hadi sasa kuomba nafasi ya kuipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha
urais, kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 25 na wengi wao wanaendelea na kazi
ya kukusanya wadhamini katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Kwa
mujibu wa ratiba iliyotolewa hivi karibuni na Katibu wa Itikadi na
Uenezi, Nape Nnauye, Kamati ya Usalama na Maadili itafanya kikao chake
Julai 8, mwaka huu kuangalia utaratibu wa kanuni kama haukuvunjwa.
Alisema
kikao hicho kitafuatiwa na Kamati Kuu itakayofanyika Julai 9 ambayo
inatarajiwa kuchuja wagombea hadi watano, kisha Halmashauri Kuu ya Taifa
(NEC) itakayofanyika Julai 10 ambayo itapunguza zaidi na kubakiza
wagombea watatu watakaopigiwa kura na mkutano mkuu.
Mkutano Mkuu wa chama utafanyika Julai 11 na 12 na kumchagua mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho.
Kwa
upande wa mgombea urais wa Zanzibar, Nape alisema Kamati ya Usalama na
Maadili ya Zanzibar, itafanya kikao chake Julai 4, ikifuatiwa na Kamati
Maalumu Julai 5.


No comments:
Post a Comment