CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Kaskazini, kimemchagua
Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho Godbless Lema, kama Kamanda wa
Operesheni ya Uandikishaji wa Daftari la Wapigakura katika kanda hiyo.
Hayo
yalisemwa juzi jijini hapa na Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha, Calist
Lazaro, alipokuwa akizungumza katika kikao maalumu cha mkakati
kilichowashirikisha viongozi wa Wilaya ya Arusha, wenyeviti wa kata na
viongozi wa Chadema wa Serikali za Mitaa kutoka kata 25 za Jiji la
Arusha.
“Tuweke
akili zetu kwenye BVR kwani hakuna ushindi bila watu kujiandikisha,
naomba nimtambulishe Lema kama Kamanda wa Operesheni ya BVR katika Kanda
ya Kaskazini, ambaye ataongoza kampeni hiyo ya kuhamasisha wananchi
wajiandikishe kwa wingi ili tuweze kushinda,”alisema Lazaro
Alisema
kutokana na uhamasishaji wa Lema ambaye pia ni Mbunge wa Arusha Mjini,
utakiswezesha chama hicho kushinda katika uchaguzi mkuu na hata kuongeza
idadi ya majimbi kutoka mawili ya sasa.
Awali
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha, Derick Magoma, alisema lengo la
kikao hicho ni mkakati ya kuhimiza wananchi kujiandikisha kwenye
daftari hilo ili kushinda katika uchaguzi huo kwa kishindo.
“Tusipojiandaa
sasamhatutaweza kushinda uchaguzi huu,kwani tumedhamiria kushinda kwa
kishindo, ndiyo maana tumeitana hapa kupanga mikakati ya ushindi ikiwa
ni pamoja na kuhamasisha wananchi kujiandikisha, mwaka huu hata walete
magari yenye maji ya kuwasha, mabomu, lakini ushindi ni lazima,”alisema
No comments:
Post a Comment