VIONGOZI WAKUU EAC KUJADILI MGOGORO WA BURUNDI DAR ES SALAAM - LEKULE

Breaking

7 May 2015

VIONGOZI WAKUU EAC KUJADILI MGOGORO WA BURUNDI DAR ES SALAAM


William Samoei Ruto, Rais Jakaya Mrisho Kikwete na wakuu wenzie wa EAC wakisimama kwa wimbo wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Ushirikiano wa Kimataifa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa, wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanatarajiwa kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kujadili mgogoro wa kisiasa unaoikabili Burundi.

Mh. Benard Membe ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Mawazir wa Mashauri ya Kigeni wa EAC.

Benard Membe, ambaye yuko Burundi akiuongoza ujumbe wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema kuwa, mkutano wa viongozi wakuu wa jumuiya hiyo unatarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Wakati huo huo, Daniel Kabuto, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Burundi amesema kuwa, ujumbe wa Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda, Tanzania, Kenya na Uganda jana uliwasili Bujumbura kwa ajili ya kusikiliza pande zinazozana nchini humo na kutafuta njia ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa nchi hiyo.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Antonio Guterres, Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ameeleza wasiwasi lilionao shirika hilo kuhusiana na mgogoro wa Burundi.

Katika kipindi cha wiki moja iliyopita Burundi imekumbwa na machafuko na ghasia kufuatia tangazo la Rais Pierre Nkurunziza kuwa atawania urais kwa muhula wa tatu. Takribani watu 13 wamepoteza maisha katika ghasia hizo.

No comments: