Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amerejea nchini humo, huku
naibu kiongozi wa mapinduzi akikiri kuwa jaribio la kumuangusha
Nkurunziza limeshindwa. Umoja wa Mataifa umetaka kurejeshwa haraka
utawala wa sheria.
Mshauri mwandamizi wa mawasiliano wa rais Willy Nyamwitwe, alisema
Nkurunziza amerejea nchini humo, lakini hakutoa maelezo zaidi kwa kile
alichosema ni sababu za kiusalama.
Nkurunziza alikuwa nchi jirani ya
Tanzania kwa ajili ya mazungumzo ya kikanda siku ya Jumatano wakati
mapinduzi yalipotangazwa na Jenerali Godefroid Niyombere, na kufunika
wiki kadhaa za maandamano dhidi ya jaribio la rais kutafuta muhula wa
tatu.
Taarifa za kurejea kwa rais Nkurunziza hazikuweza kuthibitishwa na duru
huru hata hivyo, na uwepo wake umeendelea kuwa kitendawili usiku wa
Alhamisi.
Lakini tangazo kwamba amerudi lilifuatia haraka na kukiri kwa
naibu kiongozi wa mapinduzi Cyrille Ndayirukiye kwamba mapinduzi hayo
yameshindwa.
Ndayikuriye aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP,
kuwa binafsi anatambua kuwa vuguvugu lao limeshindwa.
Wanajeshi Watiifu wadhibiti vituo muhimu
Mapema Alhamis, wanajeshi watiifu kwa rais walisema walizuwia
mashambulizi mawili makubwa yaliyofanywa na wapinzani katika mapambano
makali ya kudhibiti kituo chenye umuhimu wa kimkakati cha redio ya
taifa.
Miili ya wanajeshi watatu ilionekana ikiwa imelala mitaani karibu
na eneo la mapigano hayo, ishara ya kwanza ya maafa katika kadhia hiyo
ya mapinduzi.
Kufikia mchana, mkurugenzi wa kituo hicho Jerome Nkokirantevye alisema wanajeshi watiifu ndiyo walikuwa wanakidhibiti kituo hicho.
Kufikia mchana, mkurugenzi wa kituo hicho Jerome Nkokirantevye alisema wanajeshi watiifu ndiyo walikuwa wanakidhibiti kituo hicho.
Afisa mwanadamizi wa polisi alithibitisha taarifa hizo na kusema jana
jioni kuwa wanajeshi wanaounga mkono mapinduzi walisambaratika baada ya
mashambulizi yao dhidi ya Televisheni ya taifa RTNB na jengo la redio
katika mji mkuu kukandamizwa. Alisema baadhi ya waasi tayari
wamejisalimisha na wengine walikimbia.
Tangazo la mapinduzi la Jumatano lilisababisha ukosoaji kutoka sehemu
mbalimbali za dunia, na kuibua hofu ya kurejea katika vurugu kubwa
katika taifa hilo maskini, ambalo bado linaendelea kuhisi athari za vita
vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 vilivyomalizika mwaka 2006, na
kugharimu maisha ya maelfu ya Warundi.
Baraza la Usalama laonya
Marekani ilisisitiza Alhamis kuwa Nkurunziza ndiye rais halali wa
Burundi . Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililokutana
katika kikao cha dharura siku ya Alhamis, lililaani jaribio hilo la
mapinduzi, na kutaka kurejeshwa haraka kwa utawala wa sheria na
kufanyika kwa uchaguzi kwa kuzingatia makubaliano ya Arusha.
Katika taarifa iliyosomwa na Raimonda Murmokaite, balozi wa Lithuania
katika Umoja wa Umoja wa Mataifa, na rais wa barala hilo kwa mwezi wa
Mei, baraza hilo lenye wanachama 15 lilieza utayarifu wake kuchukulia
hatua vitendo vya vurugu nchini Burundi vinavyotishia amani na usalama.
"Wanachama wa baraza la usalama wamelaani machafuko nchini Burundi na
hasa wamewalaani wanaochochea vurugu za aina yoyote dhidi ya raia, na
wale wanaotaka kutwaa madaraka kwa njia zisizohalali," alisema
Murmokaite.
"Wanachama wa baraza la usalama wametoa wito kwa pande zote kutotumia
vurugu na kutoa kipaumbele kwa amani na usalama. Baraza pia limerejelea
uungaji wake mkono wa juhudi la mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Said
Djinnit, Umoja wa Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki."
No comments:
Post a Comment