RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI - LEKULE

Breaking

27 May 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA NNE WA MABALOZI


Mhe. Rais Kikwete akizungumza huku Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula wakimsikiliza.

Rais Kikwete akiendelea na hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine aliwakumbusha Mabalozi kuwathamini Watanzania waishio nje ya nchi, kuendelea kusaidia upatikanaji wa misaada ya maendeleo, masoko ya bidhaa za Tanzania, wawekezaji na teknolojia bora.

Sehemu ya Mabalozi wakifuatilia hotuba ya ufunguzi ya Mhe. Rais Kikwete (hayupo pichani)

Wakuu wa Vitengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifutilia hotuba ya Mhe. Rais Kikwete ambaye haonekani pichani.

Waziri Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu, Balozi Mulamula huku Balozi Sefue akisikiliza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi.

Mhe. Rais Kikwete akiwa ameongozana na Balozi Mulamula kuelekea eneo la kupata picha ya pamoja.

Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

(Picha na Reginald Philip)

No comments: