PICHA UNYAMA Jijini Mwanza: Bibi Amchoma Visu Vya Moto Mjukuu Wake Akimtuhumu Kupoteza Peni Ya Sh. 200 - LEKULE

Breaking

27 May 2015

PICHA UNYAMA Jijini Mwanza: Bibi Amchoma Visu Vya Moto Mjukuu Wake Akimtuhumu Kupoteza Peni Ya Sh. 200


eshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia bibi mmoja ajulikanaye kwa majina ya Laurencia Athanas mkazi wa Kiseke, Ilemela jijini Mwanza kwa tuhuma za kumchoma visu vya moto mjukuu wake na kumsababishia majereha mbalimbali mwilini akimtuhumu kupoteza peni ya sh. 200.

Mtoto huyo aitwaye Jackson Hosea ( 10 ) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kiseke iliyoko Ilemela Jijini Mwanza alifanyiwa unyama huo nyumbani kwa bibi huyo ambaye ni mzazi wa mama yake aishiye Nzega siku ya Ijumaa jioni tarehe 23 May 2013.

Afisa Mtendaji wa eneo hilo, Bi Hellen Mcharo ameithibitishia Mpekuzi kutokea kwa tukio hilo na kudai kwamba liliibuliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatatu ya Mei 25, 2015 na mwalimu wa mtoto huyo aliyemtaja kwa jina moja la Mwl. Midali

No comments: